Nathari

Nathari ni lugha ya riwaya ambayo si ya kishairi bali ni maelezo tu. Lugha yenyewe hupangwa bila kutumia mpangilio au ufundi wowote wa kishairi.

Nathari ni tawi moja la fasihi andishi ambalo huwa na tungo za kisanii za kubuni ambazo hutumia lugha ya kimaelezo kimfululizo na kiinsha/mjazo kupasha ujumbe wa kuelimisha, kuburudisha. Mifano ni riwaya,hadithi fupi na insha.