Tashihisi, Uhaishaji au Uhuishi

Hii ni mbinu ya kuvipa vitu visivyo na uhai sifa na tabia za ubinadamu za kusema au kutenda.Katika mfano ufuatao, chungu cha kupikia kimepatiwa sifa za binadamu kuongea. Chungu hiki kinalalamika kuwa kinatumiwa kila wakati kupikia ila hakipatiwi chakula kinachopikwa.

Mfano: Chungu Nachomeka

Mafiga umeyapanga, mekoni kuniinjika,
Kuni umeshazipanga, kwa moto ukaniweka,
Nyinginezo wazichonga, moto wako kuukoka,
Miye chungu nachomeka, nisipate hata tonge?