Jazada

Hii ni mbinu ya kutumia mafumbo ambapo mtunzi hutoa maelezo ya kitu kuwakilisha kitu kingine. Kwa mfano, ua au ndege hutumika kumaanisha mpenzi. Tausi hutumika kurejelea mtu mwenye kiburi au maringo.Katika mfano ufuatao, mtunzi anatumia neno yai kuwa mpenzi. Yai lisipowekwa vizuri huvunjika. Analinganisha mpenzi wake na yai kwa kumaanisha ahifadhiwe vyema asipate majeraha ama maovu yoyote maishani.

Mfano: Ulitunze Yai Langu

Yai langu la mahaba, lisipate kudhurika,
Kutwa moja niwe baba, vema likihifadhika,
Mwisho usitowe toba, maasi yakikutoka,
Ulitunze yai langu, lisivuje kuvunjika.