Majazi

Majazi ni hali ya kumpa mhusika, mahali au kitu jina linalofanana na tabia zake au baadhi ya sifa zake. Kwa mfano, Busara ni mutu mwenye hekima, Buraha ni mahali pa kupata furaha, Ghulamu ni kijana mwanamume na Siti ni kijana mwanamke.Katika mfano ufauatao, mtunzi anamwita mpenzi wake Siti. Siti sio jina lake halisi limetumiwa hapo tu kwa kutumia mbinu ya majazi.

Mfano: Nimeshampata Mwali

Siti amenikubali, ombi nilipompasha,
Hakuola yangu mali, upendo ulimtosha,
Ana mema maadili, tabiaze zaridhisha,
Nimeshampata mwali, pekee ananitosha!