Tashbiha au Mshabaha

Huku ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kuwa vina mshabaha au mfanano wa sifa fulani. Maneno yafuatayo ya ulinganishaji hutumiwa maneno kama; sawa na, mfano wa, ja, kama au mithili ya.Mshairi analinganisha mawaidha na ngao kwa mfano wa kwanza kwa kuwa mawaidha anayoyatumia kwenye shairi lake litamkinga mtoto/kijana kwa maovu ya ulimwengu. Katika mfano wa pili analinganisha urembo na ua kwa maana kuwa urembo huo ni muda tu, kutwa moja huisha. Mfano wa mwisho, amelinganisha maisha na ua kwa kuwa mwanadamu maisha yake huishia kifoni.

Mfano wa Kwanza: Watoto ni Baraka

Watu wana njia nyingi, wanavyolea wanao,
Kunayo mawaidha mengi, yaliyopo kama ngao,
Nielezeni kwa wingi, tunahitaji mazao,
Nataka mnieleze, mtalea mwana vipi?

Mfano wa Pili: Urembo ni Kama Ua

Ni vema kujikwatua, vizuri ukapambika, 
Jua ngozi huungua, ukabaki kuchomeka, 
Lifikalo kubabua, hiyo sura takunjika, 
Urembo ni kama ua, hujajua hunyauka!

Mfano wa Tatu: Maisha ni Kama Ua

Maisha huwa murua, hatima huharibika,
Leo hili waamua, keshoye latatanika,
Ukweli hajatambua, vema ukatambulika,
Maisha ni kama ua, kutwa moja hunyauka.