Vina

Vina ni silabi zenye sauti ya namna moja zinazotokea katikati au mwishoni mwa kila mshororo wa kila ubeti wa shairi. Kuna vina vya kati na vina vya mwisho.  

Kwa mfano, katika ubeti ufuatao, vina vya katikati ni -ka ilhali vya mwisho ni -ki.

Jambo litatatulika, iwapo halibaniki,
Halikosi bainika, faraja au la dhiki,
Lazima litasomeka, iwapo halisemeki,
Panapo moto hufuka, ishara hazifichiki.

Katika mfano unaofuata, vina vya katikati ni -ma na vya mwishi ni -ri

Nashuhudia ghanima, iliyodhaniwa shari,
Mawazo kuyasusuma, nisije itwa bairi,
Waziwazi nayasema, nisidhaniwe bakari,
Maotea hunawiri, kushangaza mkulima!