Tasifida

Tasifida ni mbinu ya kutumia maneno ya heshima na adabu kuepuka maneno ya aibu na matusi. Maneno ya heshima yanayokubalika ni kama mjamzito, makalio, maziwa, kendesha, nk.Katika mfano ufuatao, mtunzi ametumia neno maziwa badala ya matiti kwa kutumia mbinu ya tasifida.

Mfano: Nitongoze kwa mpango

Wabisha wangu mlango, chumba changu wakijuwa,
Uwazi wako mgongo, wanionesha maziwa,
Kumbe unayo malengo, wanijia kusumbuwa,
Nitongoze kwa mpango, kila mwendo ni hatuwa!