Chuku au Udamisi

Mbinu hii hutumiwa kutia chumvi maelezo ya kitu ili kutoa sifa zake zaidi. Baadhi ya maelezo huwa si ya kweli kwa kweli si lazima yatokee maishani.Katika mfano ufuatao, mbinu ya chuku imetumiwa.

Mtunzi ametia chumvi kwa kuelezea ati moyo wake unadunda na hauna hisani kwa kuachwa na mpenzi wake.

Mfano: Umeniacha Mwandani
Unadunda, moyo hauna hisani,
Ulikanda, mwili wangu kuubuni,
Langu tunda, kaanguliwa mtini,
Umekwenda, umeniacha mwandani?