Wanabiashara wadogo huumia kwa mikopo wanayopata kwa kuwa na riba kubwa. Waipate wapi karadha?
Mkopo bila riba! Karadha Nipate Wapi?


Karadha Nipate Wapi?

Kutwa ninahangaika, niko nalo hangaiko,
Inanibidi kumaka, nikakumbwa na kimako,
Nipate wapi karadha, mkopo usio riba?

Nendapo ili nikope, ni bure kwamba sikopi,
Naharibu niihepe, Kumbe riba siigepi,
Nipate wapi karadha, mkopo usio riba?

Riba imekuwa hewa, unapotaka mkopo,
Tena wameiinuwa, iso riba isiwepo,
Nipate wapi karadha, mkopo usio riba?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*