Iwapo kuna jambo moja ambalo huzuia maendeleo katika nchi, ni ufisadi. Tazama shairi hili la mwaka wa 2007. Ukabila Hatunao


Ukabila Hatunao

Jicho lake lakuona, usije sema haoni,
Usitafute laana, asije kata amani,
Vita havina maana, usije kata amani,
Mbona hunayo huruma, vita nchini kuzua?

Watu vitwa wanakatwa, damu yao kama mito,
Twalia michana kutwa, tunapochomewa vito,
Kila mara twafuatwa, tubebapo ya uzito,
Kwani hatuhurumii, kiongozi wa wahuni.

Wazalendo wanalia, vilio vinasikika,
Wakati umewadia, vilio huku Afrika,
Watu wameangamia, wazalendo wateseka,
Ukabila hatunao, Mungu wetu ni mmoja.

Walimwengu twaendapi, kwa vita vya ukabila,
Amani leo i wapi, ni wangapi wanalala?
Tapata amani vipi, kati yetu makabila,
Mola wetu atuona, japo tuna ukabila.

Kisirani na udhia, karaha na usumbufu,
Utadi watuzidia, waenea udhaifu,
Kila siku ni ramia, daima uharibifu,
Hatunalo la kusema, Mwenyezi Mungu aona.

Shelabela ni kwa wingi, hakunayo ya amani,
Kubaguana kwa rangi, mwambao hadi barani,
Umebomoka msingi, turudi tena jengoni,
Vipi tena tutajenga, jengo tulilobomoa?

© Kimani wa Mbogo (01/01/2007)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*