Yapaswa umshukuru mzazi wakati yu hai. Isingekuwa ni yeye hungekuwa katika ulimwengu huu. Mshukuru kwa lolote. Shukran Baba


Shukran Baba

Kushukuru ni lazima, wazazi niwapongeze,
Sitawahini heshima, baraka niziongeze,
Silitaki la lawama, ili mola anituza,
Heri kifo kinigwie, baba nisipopongeza.

Heshima tampatia, ili nibaki salama,
Mikono tanipungia, nimtendeapo mema,
Hatimaye sitalia, nitakuwa nayo mema,
Heri kifo kinigwie, baba nisipopongeza.

Tamsaidia vema, msaada hali mali,
Nyumbani taishi kwema, tamtunza akubali,
Ailipendi la lawama, nataka afya kwa mwili,
Heri kifo kinigwie, baba nisipopongeza.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*