Mama yako ndiye aliyekukopoa. Awapo hai, mshukuru kwa lolote lile. Shukran Mama


Shukran Mama

Si haba miezi tisa, mwanao kuvumilia,
Hicho ndicho changu kisa, pongezi kukupatia,
Nashukuru hivi sasa, nasaha kunipakia,
Heri nife kwa mashaka, mama nisipokusifu.

Shukurani napakua, wewe nikuandalie,
Kwa sasa nimegundua, hisani nikupatie,
Msondo nauchukua, wimbo wangu nikwimbie,
Heri kifo kinigwie, mama nisipopongeza.

Koja langu nakuvika, lililorembeshwa sana,
Zawadi nyingi hakika, kwenye kikapu kipana,
Maneno nayatamka, akubariki rabana,
Heri kifo kinigwie, mama nisipopongeza.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*