Aliyependwa akiondoka, watu husononeka na sifa kumumiminia. Huu mfano wa shairi la Tanzia Hatuna la Kusema

Hatuna la Kusema

Tunayo nyingi huzuni, hakika twasikitika,
Mwalimu wa kanisani, ni tuzi aliondoka,
Twahuzunika nyoyoni, Joyce tukimkumbuka,
Hatunalo la kusema, bali Mungu twashukuru.

Alitufunza injili, mambo mema ya imani,
Katufunza maadili, wema usio kifani,
Katuonyesha fadhili, ili tuwena hisani,
Hatunalo la kusema, bali Mungu twashukuru.

Pengo kubwa litabaki, atakumbukwa daima,
Nyoyoni mwetu hatoki, Joyce bingwa wa heshima,
Wema kwa Mungu ubaki, Muumba wa watu wema,
Hatunalo la kusema, bali Mungu twashukuru.

Japo nyoyo tuna shaka, twakusifu ufahari,
Mwalimu umeondoka, mwalimu Joyce kwa heri,
Twamshukuru Rabuka, kutupa mtu hodari,
Hatunalo la kusema, bali Mungu twashukuru.

Mwisho wetu tumefika, wema wako twaheshimu,
Mbinguni takapofika, taonana kwa Rahimu,
Twabaki kusononeka, kwa heri Joyce mwalimu,
Hatunalo la kusema, bali Mungu twashukuru.

© Kimani wa Mbogo (24/05/2008)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*