Anapoajiliwa, atafuata amri za bosi. Akikosea, atakuwa akikaribisha cheche kali za maneno yatakayomkera na kumdunisha. Simba Akishanguruma


Simba Akishanguruma

Waoga waajiriwa, bosi kukabili,
Leo aje amelewa, bila maadili,
asubuhi kuchelewa, nani atakuli,
Simba akishanguruma, nani achezaye?

Vingi vitisho alete, wingi wa matusi,
kukejeli asisite, anapojasisi,
Nani aende apite, karibu na bosi?
Simba akishanguruma, nani achezaye?

Umkutapo ofisi, mabaya ataje,
Usowe usianisi, mema asitaje,
Akishaogopwa bosi, kazi ifanyweje?
Simba akishanguruma, nani achezaye?

Hoja gani kuitupa, mja kama wewe?
Bora kazi kuitupa, asiogopewe,
Huyo mwenye kukulipa, ndiye kama mwewe?
Simba akishanguruma, nani achezaye?

© Kimani wa Mbogo (01/01/2007)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*