Hufai kunishutumu wala kunilaumu kwa tukio lililo kadri ya uwezo wangu. Yote ni yaMungu na yeye tu ndiye mwenye uwezo. Mbona Wanishutumu?


Mbona Wanishutumu?

Unanishutumu, ulo mwana wa ugeni,
Unanishutumu, kipi chako cha jubuni?
Unanishutumu, unajisahau kwani?
Unanishutumu, sote tulio kazini,
Unanishutumu, kwa nini wanishutumu?

Unanishutumu, kwa kunitia aibu,
Unanishutumu, waniudhi kwa ghadhabu,
Unanishutumu, kwahicho changu kitabu,
Unanishutumu, kunishutumu ajabu,
Unanishutumu, kwa nini wanishutumu?

Unanishutumu, kwa kweli uneni sina,
Unanishutumu, kwa kazi yangu bayana,
Unanishutumu, wajijua wewe mwana,
Unanishutumu, ujifanyaye mtwana,
Unanishutumu, kwa nini wanishutumu?

Unanishutumu, kiwango cha kushutumu,
Unanishutumu, wajidhani utadumu,
Unanishutumu, wewe unayehudumu,
Unanishutumu, kwa kweli wanilaumu,
Unanishutumu, kwa nini wanishutumu?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*