Kunao baadhi ya watu hawapendezwi na chochote unachokifanya. Usivunjike moyo. Watakudharau tu leo lakini kesho watakuhitaji. Tenda wena nenda zako! Nifanyalo hulioni


Nifanyalo hulioni

Walisemalo hukani, nilisemalo wakana
Lilarukalo hushoni, lisoraruka washona
Nifanyalo hulioni, nisolifanya waona.

Kaziyo bwana sitaki, uhuru kwangu nataka,
Usotupa yetu haki, tusiwe nayo baraka,
Ya kudumu hunipaki, tope jingi menipaka,
Nifanyalo hulioni, nisolifanya waona.

Mtu mukubwa haniti, kitoto ananiita,
Atumia chake kiti, asemapo sijakita,
Lango kuu hapiti, akijua tanipita
Nifanyalo hulioni, nisolifanya waona.

Maishangu menda komba japo pojo mfukoni,
Kooni tafunga kamba, ning’inie mnazini,
Kuzimu nende kutamba, niondoke maafani,
Nifanyalo hulioni, nisolifanya waona.

Maoni 1 kwa “Nifanyalo hulioni”

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*