Furaha huwa furaha wakati unaohitajika. Huwi na furaha kulazimishwa ila ni jambo linalotokana na mawazo yako. Bongo Zikichangamka


Bongo Zikichangamka

Wanao uchangamfu, usioridhisha,
Watajipanga kwa safu, wakiadhimisha,
Wajigambe wajiswifu, kujikadirisha,
Bongo zikichangamka!

Mambo yasiyokifu, kujidhihirisha,
Katu hawawi na hofu, kujichangamsha,
Akili zao dhaifu, kujihusudisha,
Bongo zikichangamka!

Hudhani wako nadhifu, kujikabilisha,
Watu wenye majiswifu, wasioridhisha,
Mara wana ufurufu, wakijionesha,
Bongo zikichangamka!

Maoni 2 ya “Bongo Zikichangamka”

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*