Uzee ni dhahabu. Ndivyo walivyosema. Wakati mwingine utategemea muda ulioishi duniani ili kuongozwa na matukio yaliyopita. Mara yakupe nguvu na mara yakuvunje moyo. Jiwe Lenya Uzulufu


Jiwe Lenya Uzulufu

Waambiwapo huhema,
Wanapolala huhema,
Waulizwapo husema,
Jiwe lenye uzulufu.

Walimwengu hutafuna,
Daima hufarakana,
Dawamu huliguguna,
Jiwe lenye uzulufu.

Jiwe lenye uzulufu.
Jiwe la umaarufu,
Mara la ulaanifu,
Jiwe lenye uzulufu.

Jiwe jeusi hakika,
Katu liso na baraka,
Jiwe lililotukuka,
Jiwe lenye uzulufu.

Daima watalisifu,
Jiwe lenye usumbufu,
Jiwe lenye ukalifu,
Jiwe lenye uzulufu.

Watalisifu daima,
Jiwe jeusi la zama,
Waulizwapo husema,
Jiwe lenye uzulufu.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*