Usitazame mtu kiatu alichovaa ukamdharau au kumkosea heshima. Aidha usifanye hivyo kwa mavazi yake, Kiatu Cha Malenga


Kiatu Cha Malenga

Kiatu changu aali, makubadhi nipendacho,
 Nani huyo atakuli, anidharau kwa hicho?
 Nionwaye baradhuli, na wale wenye kificho,
 Nani asemaye leo, Makubadhi si kiatu?

Njuti zangu nivaapo, mguu kuufunika,
 Hilo liitwalo kopo, waonalo kama taka,
 Hao wanipuuzapo, miguu nikifunika,
 Nani akuliye leo , kwamba njuti si viatu?

Buti langu nililivae, waniona kama juha,
 Nikisema wakatae, ati lile ni la juha,
 Watakao niyatwae, mabuti yangu ya raha,
 Nani aambaye leo, kwamba buti si kiatu?

Kiatu changu malenga, wakitazamia nini?
 Uonapo nikitanga, tazamo wanipa lani?
 Wanifanyao mjinga, kuniona miguuni,
 Nani akataye leo, kwamba ndara si kiatu?

Wataka uone changu, wakati wa kulahiki,
 Makuhbadhi yalo yangu, kuyaona hawataki,
 Nikivaa njuti zangu, hakuna mtu hacheki,
 Nani atakayesema, malenga hana kiatu?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*