Kila mtu hujua vifaa vyake vya kazi. Fundi ana vyake. Je wavijua? Fundi Usinipuuze


Fundi Usinipuuze

Bisibisi naijua, parafujo kukazia,
Kufunga na kufungua, kutoka na kuingia,
Bisibisi nimejua, ubongoni nimetia,
Fundi usinipuuze, navijua vyombo vyako.

Utakapo chombo chema, mbao kulainisha,
Ndivyo mbao ziwe njema, randa kulainishia,
utalainisha hima, mbao kusawasishia,
Fundi usinipuuze, navijua vyombo vyako.

Mbao zako kupasua, wahitaji msumeno,
Chombo hicho nakijua, nalijua kila neno,
Huo utauchukua, nakupatia mfano,
Fundi usinipuuze, navijua vyombo vyako.

Balari utaendea, pia huitwa patasi,
Mashimo kutombolea, utaendea churusi,
Mbao tundu kuwekea, utatunia patasi,
Fundi usinipuuze, navijua vyombo vyako.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*