Ni vema kusikiliza waadhi kutoka kwa wakuu wako. Wasikilize na utende kwa mujibu na wanaokushauri, Haya Katu Siyapinge


Haya Katu Siyapinge

Uwaonao jichunge, ufikirio laini,
Hatima ukajikinge, nao wenye kulaani,
Haya katu siyapinge, sikufichi, mathalani,
Hata wote wakupinge, maarifa jisheheni.

Uwadhanio wanyofu, unyofu wale hawana,
Wonao watakatifu, utakakitu maana,
Walio uadilifu, wote ndo wafarakana,
Walio nyoyo kunjufu, ndaniyo usowaona,

Ushuhudio wazima, maradhi yao ni mengi,
Walio safi mitima, wanayo nyeusi rangi,
Waonyeshao kuvuma, ubayao ulo mwingi,
Walo wazuri kusema, wa domo kaya ndo wengi.

Kwa unyofu watendao, ndo hao wapingamizi,
Kwa bidii wafanyao, ndo waharibuo kazi,
Wakulima uwonao, ndo huchimbua mizizi,
Makaziyo uwekao, ndo wengi walio wezi.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*