Mbona nasononeka hivyo moyoni? Kwa nini nahangaika hivyo ndani mwangu? Nitamtumainia Mungu, maana nitamsifu tena yeye aliye msaada wangu na Mungu wangu. ~ Zaburi 42:5 Ni Furaha Iliyoje?


Ni Furaha Iliyoje?

Uendapo kotekote, hulioni tumaini,
Iwapo ukatafute, utakosa tumaini,
utembeapo upate, hulipati tumaini,
Ni furaha iliyoje, kuwa nalo tumaini!

Magharibi uendapo, hulioni tumaini,
Mashariki ufikapo, utakosa tumaini,
Kusini utafutapo, hulipati tumaini,
Ni furaha iliyoje, kuwa nalo tumaini!

© Kimani wa Mbogo (01/01/2008)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*