Twaipenda shule yetu, twaisifu kwa umoja,
Twapenda masomo yetu, hili sasa twalitaja,
Shule njema yetu, daima nambari moja,
Mambo yote tufanyayo, shule yetu twaongoza.
Walimu wetu ni wema, twawasifu kwa shairi,
Wametufunza heshima, kila siku tuna heri,
Ndivyo wima twasimama, tuutangaze uzuri,
Mambo yote tufanyayo, shule yetu twaongoza.
Wazazi twawapongeza, kwa makini sikizeni,
Wasiwasi twatangaza, masikio yategeni,
Peke yetu twaongoza, twang’ara kwetu shuleni,
Mambo yote tufanyayo, shule yetu twaongoza.
© Kimani wa Mbogo (01/01/2008)