Piga moyo konde. Jipe nguvu maishani. Usife moyo, Mungu hatamsahau mja wake. Ninatangaza!


Ninatangaza!

Ninatangaza!
Nitatumia maneno yangu kubariki,
Nitatangaza ushindi kwa familia yangu,
Wema na fadhili zitanifuata.

Ninatangaza!
Vile nitasaidia walio karibu nami,
Ili wafaulu maishani mwao,
Vile najivunia Ushindi wao.

Ninatangaza!
Ya kwamba nitawapenda daima,
Niwaambie umuhimu wao,
Ushindi na urembo walio nao.

Ninatangaza!
Watafanya makuu maishani,
Kwa imani wanao uwezo,
Wametakazwa na wamejihami.

Ninatangaza!
Hakuna kizuizi kitanikwaza,
Mawazo yangu yanaongozwa na Mungu,
Akili zangu zimeratibiwa kwa ushindi.

Ninatangaza!
Mungu ana mipango bora ya maisha yangu,
Anaziongoza nyayo zangu,
Hufanya juhudi zote kwa manufaa yangu.

Ninatangaza!
Kielelezo cha imani maishani mwangu,
Maisha yangu yana alama ya ushindi,
Wingi wa baraka za Mungu utanizunguka.

Ninatangaza!
Kwamba nina neema ninayohitaji,
Wingi wa nguvu na uwezo,
Nitaruka vikwazo vyote,
Na nishinde majaribu yatakayoniandama.

Ninatangaza!
Mungu atanifungulia milango ya baraka,
Ataandaa watu wema maishani mwangu,
Baraka nazo hazitakoma kuniandama.

© Kimani wa Mbogo (18/01/2019)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*