Uyaole ya dunia, hangaiko yasikupe,
Kwayo mazuri tulia, usije kuwa mapepe,
Uwe mwema kwa tabia, daima moyo ujipe,
Nakupa wangu wasia!
Mwanangu usijipende, kwa mwenendo uwe mwema,
Maisha ukayashinde, kwa hishima na huruma,
Kwa raha usijiponde, zikakuweza tuhuma,
Nakupa wangu wasia!
Enenda shule kusoma, elimu ikuongoze,
Jizolee kubwa dhima, kutenda mengi uweze,
Usiwate taadhima, kila kutwa itukuze,
Nakupa wangu wasia!
Furahi ufurahie, kwa hekima ujipambe,
Waja wakutamanie, unavyokosa uzembe,
Pa ibada uingie, mfinyanzi akuumbe,
Nakupa wangu wasia!
Utafute mke mwema, uoe na kumpenda,
Ikuongoze neema, malezi bila kudinda,
Maovu ukiyatema, mema nayo kuyatenda,
Nakupa wangu wasia!
Shairi jema sana la mzazi kwa mwanawe.
Asante sana Neema
Hata Mie NAOMBA mnifunze jinsi ya kutunga na kuchambua shairi
Tuandikie tukujuze Zaidi. Baruapepe: mwanagenzi@gmail.com
Inahimiza sana na Lina maudhui mazito kwetu wazalendo
Asante sana kwa mchango wako wa maoni na tathmini.
Napenda hili niongoze NAMI pia
Naitaji shairi Umuhimu wa bima ya afya