Walisema jogoo wa mashambani hawiki mjini. Unapotoka mashambani na kuingia jiji, lazima uziwache tabia ulizokuwa ukifanya awali. La sivyo, watakucheka! Kuhama Kitongoji


Kuhama Kitongoji

Nisaidie Karima, kutenda yalio mema,
Nataka niweze hama, hiki kijiji kwa hima,
Kijiji cha wanachama, wa matendo yaso mema,
Kitongojini kulima, dhambi na yasiyo mema.

Mtu aliyezaliwa, kwa Mola hubarikiwa,
Hupewa chake kipawa, kujilinda kwa ukiwa,
Mwadilifu kugusiwa, asiweze sawasawa,
Abaki yu ufidiwa, baraka zake akawa.

Kutunukiwa hedaya, niipate bila haya,
Zisimuliwe hekaya, Masihi yake himaya,
Kuipata si vibaya, na kuwa nacho kinaya,
Kupewa naye Mesaya, kutoka kwa yake himaya.

Natazama kijijini, wimbo huu kuughani,
Ni mengi yalio ndani, na wengi kitongojini,
Waasi wenye uhuni, kafungiwa kwa husuni,
Watundu na wakunguni, furaha yao ugoni.

Hakika hiki kijiji, ni wengi wanaohama,
Wao mie nawahoji, kwa nini wao hawaji,
Hujitokeza kwa jiji, wao kuwa na ujaji,
Hao wanakitongoji, fanaka hawataraji.

Ufanisi unikifu, kwako uwe utukufu,
Baraka zije kwa safu, moyo uwe mkujufu,
Kwa mambo ya uraufu, yasiwe uharibifu,
Yasiwe na upungufu, daima nisije hofu.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*