Ndiye anayetegemewa! Ndiye kiongozi wa himaya. Anaponyamaza ni sawa na kasri kuwa mahame. Nena jambo moja tu tukusikilize! Kasri ni Mahame


Kasri ni Mahame

Ninatanabahi, kume kasri i wazi,
Tangu asubuhu, kweli imebaki wazi,
Ningeawasabahi, katika yao makazi.

Hawako makazi, pale warangapo panya,
Kasri i wazi, watawalao ni panya,
Waloachwa kazi, panya wanatarakanya.

Hii jamhuri, wengi wanatarazaki,
Vita vyakithiri, wafa na wengi wabaki,
Ni yao hiari, walofanya itifaki.

Wengi waasiri, haupo wake uneni,
Subiri subiri, bubu atoa uneni,
Ngoja manowari, toka ng’ambo i njiani.

Imetabaradi, kasri imetulia,
Aliishadidi, mwenyewe akidhania,
Aliye stadi, kweli wa ubaharia.

Ameshaabiri, Ububwi kaenda huko,
Kaiacha shari, viziwani kenda huko,
Kaacha shauri, panya kaachiwa tuko.

Kenda visiwani, kasri peke kaacha,
Kenda Ububwini, vitimbakwira kaacha,
Yuko visiwani, wameo amewaacha.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*