Unapomtakia mwenzako mema, bila shaka atafurahia na kuwa na moyo wa kuendelea licha ya changamoto atakazozipata. Koja la Ushindi


Koja la Ushindi

Langu binamu si ngano, bali ni hili shairi,
Zangu hizi beti tano, zitakazovunja shari,
Kutia nguvu ukani, kwa kukutunukia heri,
Dhibitisha uhodari, nakutakia fanaka.

Natunga huu ukara, wa kukutia heri,
Baraka ziwe ishara, uupate ujasiri,
Jitwike hii taswira, baraka kuzibusuri,
Dhibitisha uhodari, nakutakia fanaka.

Kiwewe usijitwike, mtihani kusubiri,
Ujasiri jipachike, ujisheheni saburi,
Diposa ukaridhike, na hiyo yako dhamiri,
Dhibitisha uhodari, nakutakia fanaka.

Fasihi kukutambua, kakamia ufahari,
Ubomoe kitumbua, mwishowe utakabari,
Kiu nacho kuchambua, kwa yote bila dosari,
Dhibitisha uhodari, nakutakia fanaka.

Malenga mwenye hisani, natia nanga dhahiri,
Naomba dua mwendani, baraka uwe kwa fori,
Fanana kwa mtihani ziwepo kwako janbari,
Dhibitisha uhodari, nakutakia fanaka.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*