Wakati mwingine askari hukosa ujasiri wa kutosa. Hutegemea silaha alizo nazo na Mungu wake tu. Kila wakati hujilinda na kujaribu kadri ya uwezo wake. Mwanakikosi Ayumbaye

Mwanakikosi Ayumbaye

Mwanakikosi aliya, ayumbayumba msitu,
Usiku usio kaya, hakika pasipo mtu,
Pasipo wa kuchukiya, asiye karibu katu,
Kwa visivyo vyake vitu, mwanakikosi agwaya.

Kilio nakisikiya, chake aliye msitu,
Usalama u pambaya, wa mwanakikosi mtu,
Chozi usoni atiya, kwa visivyo vyake vitu,
Kwa visivyo vyake vitu, Mwanakikosi agwaya.

Maulana aliliya, achungapo vyao vitu,
Wapenda kaya kaya, sebule walo watatu,
Lango kavika pasiya, wahakika ja upatu,
Kwa visivyo vyake vitu, mwanakikosi agwaya.

Ayumba msitu pasipo watu,
Wanyama wamliliya, vifaru, chui na chatu,
Yake iliyo hisiya, hatari ilo msitu,
Kwa visivyo vyake vitu, mwanakikosi agwaya.

Mitambo jicho tupiya, usiku kote msitu,
Hatambui palo njiya, papitwapo kwa viatu,
Kiunoni yatuliya, sime ilojaa kutu,
Kwa visivyo vyake vitu, mwanakikosi agwaya.

Mwanakikosi agaya, ahofu pigo kitutu,
Lolote ahusudiya, litendwalo kwa msitu,
Kajifunika ukaya, kwa baridi ilo butu,
Kwa visivyo vyake vitu, mwanakikosi agwaya.

Yunifomu yampwaya, mwanakikosi wa mwitu,
Hilo lake kumbwaya, vazi lake mwanamwitu,
Panapokuwa payapaya, alalapo mwanamwitu,
Kwa visivyo vyake vitu, mwanakikosi agwaya.

Mwanakikosi agwaya, kwa wa bunduki mtutu,
Aliyeiacha kaya, kuwalindia misitu,
Mwana mlinda umbeya, na mitambo ilo mwitu,
Kwa visivyo vyake vitu, mwanakikosi agwaya.

Kwa kweli awayawaya, adui asidhubutu,
Hakika apayapaya, kuwalinda walo mwitu,
Kwake aikia puya, dhidiye mlinda mwitu,
Kwa visivyo vyake vitu, mwanakikosi agwaya.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*