Unapoitumia rununu yako, jiulize atakavyoitumia bubu au kiziwi. Shairi hili la beti tatu linaelezea mengi. Rununu kwa Vilema


Rununu kwa Vilema

Huyo mpigie simu, kusikia tasikia,
Atakuwa nayo hamu, ujumbe kukupashia,
Iwe ni simu adhimu, vipi ataitumia?
Bubu asiyeongea, tatumiaje rununu?

Kiduko asesikia, simu yake ndiyo gani?
Utakapo kumwambia, haelewi sikioni,
Wakati ukiwadia, ujumbe uwe bongoni,
Kiziwi asesikia, tatumiaje rununu?

Macho yake ni dhaifu, kwona simu asiweze,
Umemwingia upofu, japo tu asikilize,
Haja vipi taikifu, waziwazi nieleze,
Kipofu asiyeona, tatumiaje rununu?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*