Usijione unajua kutunga mashairi ukaona wengine hawawezi. Shairi hili linakemea majisifu. Subiri wengine wakusifu na waelezee kama wajua kutunga! Kutunga Kuna Nini?


Kutunga Kuna Nini?

Kama nyuni huniwinga, wakinitakia shari,
Kwa mafumbo hunilenga, mara kuiweka siri,
Dhihaka watazipanga, ili nikose shamiri,
Siwi bingwa siwi bunga, kwa kutunga mashairi!

Ameniwezesha Mola, kudura zake za heri,
Vina nimevitawala, vikakubali urari,
Makitaba nimeola, kuchambua mashairi,
Yangekuwa ni chakula, ningeyala nishakiri!

Silazimishwi kufanya, ninatunga kwa hiari,
Ninatunga kuonya, sijayaweka kwa siri,
Nelimisha na kukanya, tukizi ninabashiri,
Kutunga si kupokonya, kuhifadhi mashairi.

Wazi nimejioneya, nikasikia dhahiri,
Niwapo nao ubaya, kwa kutunga sighairi,
Sasa najizubaliya, kujikunyata kwa mori,
Heri ninejitungiya, kuliko weye jasiri.

Unapojua kutunga, hujifanza wanawiri,
Hujavipata vimbunga, viweze kukuathiri,
Hivi vina kuvikonga, vinataka umahiri,
Havitakiwi vya ujinga, ukenda zako hubiri.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*