Waliosema masomo sio “Suruali” hawakuna na la kutafakari. Kwa sasa elimu ni mali na kila mtu ameuona umuhimu wake. Elimu Ni Mali


Elimu Ni Mali

Kote uendapo, elimu ni mali,
Lote usemapo, wote wakubali,
Shuleni ujapo, watafuta mali,
Elimu ni mali, leo twatangaza.

Elimu elimu, kesho iwe mali,
Jambo la muhimu, twasema ukweli,
Shuleni mwalimu, tupatie mali,
Elimu ni mali, leo twatangaza.

Pamoja twasema, elimu ni mali,
Elimu ninjema, semeni ukweli,
Sema kwa heshima, wote wakubali,
Elimu ni mali, leo twatangaza.

© Kimani wa Mbogo (01/01/2006)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*