Visawe vya “Paa”. Kila ubeti na maana moja ya neno paa. Soma shairi hili ung’amue maana tano za “paa”. Maanake Paa


Maanake Paa

Kisu kutumia, mamba kuparuza,
Usafi kutia, papa au pweza,
Muda kuwadia, samaki paruza,
Iyo hiyo ndiyo, maanake paa.

Kwa sasa igiza, jifanye yu nyuni,
Mwenyewe onyeza, tuende angani,
Mbinguni angaza, huko mawinguni,
Iyo hiyo ndiyo, maanake paa.

Makaa chukuwa, utoe mekoni,
Pweza atakuwa, uwe hatarini,
Kaa hupaliwa, kuwa tazizoni,
Iyo hiyo ndiyo, maanake paa.

Mnyama porini, mbuzi usimwite,
Pembe za kichwani, huyo umpate,
Umwone mwituni, yule asisite,
Iyo hiyo ndiyo, maanake paa.

Jenga nyumba ewe, juu tafunika,
Bati, kuti, jiwe, moja utaweka,
Nyumba njema iwe, iliyonjengeka,
Iyo hiyo ndiyo, maanake paa.

© Kimani wa Mbogo (01/01/2006)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*