Baada ya kufanya kampeni na kuwa kiongozi, mwanasiasa analalamika kuwa hajapata muda wa kutulia. Ni shida ya uongozi, Adha ya Adhama. Adha Ya Adhama


Adha Ya Adhama

Kiongozi mwaniita, jambo ambalo sikani,
Heshima pia napata, toka bra hadi pwani,
Nilipoanza kupata, nasikitika wazoni,
Kwa nini ewe dunia, uliye mzito kwangu?

Kiongozi nilidhani, ufurufu yeye huwa,
Nilikosea lakini, sina raha nilojuwa,
Siasa na kampeni, mwenyewe nilijaliwa,
Hii adha ya adhama, yaniongezea kero.

Kila siku lalamiko, lanikuta afisini,
Hakunalo badiliko, juhudi zangu huzuni,
Kwangu mimi ni kimako, silipati la thamani,
Hii adha ya adhama, yaniongezea kero.

Kura mlinipa mimi, ivumayo haidumu,
Ni kweli kipya kinyemi, ingawa kidonda damu,
Kazi nyingi kwangu mimi, haya yangu majukumu,
Hii adha ya adhama, yaniongezea kero.

Ujumbe usitamani, kigezo cha kutamani,
Hili nawaabieni, kutoka kwangu kinywani,
Dhana yangu siwahini, haya yangu madhumuni,
Hii adha ya adhama, yaniongezea kero.

© Kimani wa Mbogo (01/01/2007)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*