Mwanadamu hupitia mengi maishani. Upo wakati anapohisi kama hafai kuishi. Wakati huo atahitaji mwengine wa kumtia moyo. Siku Ya Kufa Kwangu


Siku Ya Kufa Kwangu

Walisemalo hukani, nilisemalo wakana,
Lirarukalo hushoni, lisoraruka washona,
Nilifanyalo huoni, nisolifanya waona,
Heri sasa nijiue, sina changu cha maana.

Kaziyo bwana sitaki, uhuru wangu nataka,
Usotupa yetu haki, tusiwe nayo baraka,
Ya kudumu hunipaki, tope tosha menipaka,
Heri sasa nijiue, sina changu cha maana.

Mlinzi haniiti, kitoto aniita,
Atumia chake kiti, asemapo sijakita,
Lango kuu hapiti, akijua tanipita,
Heri sasa nijiue, sina changu cha maana.

Maishangu menda komba, ngawa pojo mfukoni,
Kooni tafunga kamba, ning’inie mnazini,
kuzimu nitakutamba, niondoke maafani,
Heri sasa nijiue, sina changu cha maana.

© Kimani wa Mbogo (01/01/2007)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*