Kabla ya kuzikuza lugha za kigeni, anzia ya kwenu. Ipende lugha yako kama kuliko unavyozipenda za kigeni. Ufasaha Tuukuze


Ufasaha Tuukuze

Lugha yetu taadhima, mwaiwekea mipaka,
Hizo nyingine heshima, mwaipa na kujitwika,
Swahili jaha mwanyima, zenu mbele mwaziweka,
Lugha yetu taadhima, tuifanye kutukuka!

Lugha tukufukuvuma, yatakiwa kutukuka,
Wanafunzi wakisoma, tuiswifu kwa hakika,
Walimu mfano mwema, nao wawe bila shaka,
Lugha yetu taadhima, tuifanye kutukuka!

Tuuwache uhasama, lugha kutoeleweka,
Ghulani kwa maharima, tuifanye kutuka,
Habari hizi kuvuma, lugha mbele kuiweka,
Lugha yetu taadhima, tuifanye kutukuka!

Sheng”i yeni ni hitima, ile si lugha hakika,
Ni yao waso heshima, kweleweka wasotaka,
Kijifanya wa hekima, pasha pasi toa haka,
Lugha yetu taadhima, tuifanye kutukuka!

Masa husema ni mama, maana ovu hakika,
Demu ni siti husema, nguo iliyopasuka,
Enyi wacha uhasama, lugha yenu ilo shaka,
Lugha yetu taadhima, tuifanye kutukuka!

© Kimani wa Mbogo (01/01/2007)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*