Usibaki kunyamza. Nena tu neno moja. Bubu hana uwezo wa kusema. Wewe unaweza. Sema tu neno moja. Lumba Usiwe U Bubu


Lumba Usiwe U Bubu

Lumba neno la dhahabu, kwa mashiko ya uneni,
Lumba liwalo thawabu, ulinene kwa makini,
Lumba vema uhutubu, uliseme la thamani,
Lumba usiwe u bubu, tujue unachobuni.

© Kimani wa Mbogo (18/10/2017)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*