Je, wajua waliolemaa pia wanazo haki zao? Tazama shairi hili. Wimbo Wa Vilema


Wimbo Wa Vilema

Sisi wanakulemaa, tuna mengi ya kusema,
Tumekumbana na baa, na kuumbuka mitima,
Shida zetu twasemaa, tukishika zetu tama,
Tunayo mengi kusema, sisi tuliolemaa.

Sii kuitwa vilema, twaona kutokomaa,
Imara tumesimama, ubaguzi twakataa,
Kutaka njema huduma, pamoja sote twakataa,
Sisi tuliolemaa, tunayo mengi kusema.

kampeni twaandaa, dhidi ya hiyo dhuluma,
Huku kwetu kulemaa, twaitaka taadhima,
Tupewe kila wasaa, sisi waja wa huruma,
Tunayo mengi kusema, sisi tuliolemaa.

Maneno kuyaandama, twasimama kishujaa,
Tunaiomba neema, hatuitaki hadaa,
kuupinga uhasama, tumeikataa dhaa,
Sisi tuliolemaa, tunayo mengi kusema.

© Kimani wa Mbogo (01/01/2007)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*