Maadili Yamekosa
Mambo yamebadilika. Si kama zama zile. Maadili, taadhima na tamaduni hazipo tena. Twaelekea wapi? Maadili Yamekosa
Kitovu cha Ushairi, Washairi na Mashairi
Mambo yamebadilika. Si kama zama zile. Maadili, taadhima na tamaduni hazipo tena. Twaelekea wapi? Maadili Yamekosa
Mapenzi ni jambo la mtu na hiari yake. Hulazimishwi kumpenda huyu ama yule. Wengine watakuvunja moyo na kukwambia unayempenda si mwema. Kila mtu ana ila zake. Hakuna mwanadamu aliye kamili asilimia mia moja. Unapozitambua ila za mke wangu, jua na usinipashe kwa kuwa nilizijua kitambo. Wengine watakupasha mengi yasiyo na maana wala ukweli kuhusu mpenzi wako ili umwache amtongoze. Mara nyingi udaku hupotosha na kuangamiza wawili wapendanao ama hata familia.
Shairi lifuatalo la tarbia lina mengi ya kufahamisha. “Sijali mnavyomwita, kwangu huwa maridhia”. Hata mseme, mmbadike majina ama mmdharau, kwangu nampenda tu. Mpenzi wa mtu ni mpenzi wake tu yawache ya kwao huyawezi. Hebu lisome na utafari kwa kina. Ufurahiae uhondo wa shairi hili la Kimani wa Mbogo analoliita “Kwangu huwa maridhia”. Kwangu Huwa Maridhia
Ndoa ni jambo la muhimu linalostahili hekima na busara. Ni jambo linalofaa na kustahiki uaminifu. Mheshimu, mtunze na umfae. Mke Unaye Nyumbani
Unapoliona wingu jeusi, si maana kwamba mvua itanyesha. Inapoiona dalili, si lazima iwe ishara ya jambo fulani kutendeka. Ukweli huu unadhibitishwa na shairi hili. Wingu Jeusi Kutanda
Peke yako hutaweza bila kuungana na wenzako. Hivi ni sawa na vile jiwe moja haliinjiki chungu. Usijitie hamnazo mambo ya mwenzako. Huenda ukamhitaji. Shirikiana na wengine, uwafae nao wakufae. Moja Haliinjiki Chungu